EastAfricaTV(@eastafricatv) 's Twitter Profile Photo

Wananchi wametakiwa kuendelea kuchukua tahadhari kufuatia taarifa ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuripoti uwepo wa mgandamizo mdogo wa hewa katika Bahari ya Hindi mashariki mwa pwani ya Mtwara.

account_circle
EastAfricaTV(@eastafricatv) 's Twitter Profile Photo

Waendesha bodaboda mkoa wa Dar es Salaam, wameiomba Serikali kufunga kamera za usalama barabarani ili kuwavumbua madereva wote wenye tabia ya kusababisha ajali na kukimbia.

Mariam Shabani

account_circle
EastAfricaTV(@eastafricatv) 's Twitter Profile Photo

Kwenye ya tulisema,
“Kama sio mimi basi ni wewe, jamaa yako au mwanafamilia kikokotoo kinakuhusu ni suala la muda tu.”

Hali itakuaje kama kikokotoo kikiwahusu na Wabunge na wao walipwe nusu ya mafao yao baada ya kumaliza kipindi chao cha Ubunge...yaani walipwe…

account_circle
EastAfricaTV(@eastafricatv) 's Twitter Profile Photo

Inaonekana malalamiko ya wanaume kufanyiwa 'vitendo vya ukatili na wenza wao' vinazidi kuongezeka,
Wapo waliyopigwa, waliyoachwa kwa sababu ya maradhi au uchumi kuyumba.

Je! wanaume wenyewe ndio tatizoi?...au tatizo ni nini?

Jumatano hii kwenye ya mmoja wanaume…

account_circle
EastAfricaTV(@eastafricatv) 's Twitter Profile Photo

Hamis kavila maarufu kama Father Queen Mkazi wa Mwananyamala jijini Dar es Salaam, ameiomba imsikilize matatizo yake unahisi ana jambo gani?

cc Mariam Shabani
SAA1

account_circle
EastAfricaTV(@eastafricatv) 's Twitter Profile Photo

Jeshi la polisi mkoani Mwanza linamshikilia Jackson Kalamji mwenye umri wa miaka 49 mkazi wa Kijiji cha Mwamanyili wilayani Sengerema, baada ya kumuua mkewe, Mariam Bulacha mwenye umri wa miaka 42 kwa kumchoma na visu sehemu mbalimbali za mwili wake.

account_circle
EastAfricaTV(@eastafricatv) 's Twitter Profile Photo

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jeneral Rajabu Mabele Ameagiza Vijana Wote wanaohitimu mafunzo ya Kijeshi, Kutumika kusaidia Taifa katika kudumisha amani kwa Watanzania, na kujiepusha na matumizi ya dawa za kulevya.

account_circle
EastAfricaTV(@eastafricatv) 's Twitter Profile Photo

VIJANA WAPEWA MBINU YA JINSI YA KUJISHUGULISHA.

Wakati leo ikiwa ni siku ya wafanyakazi duniani, vijana wameaswa kuwa shughuli za kufanya zipo na kwamba hakuna haja ya kukaa kijiweni na kufanya uhalifu.

account_circle
EastAfricaTV(@eastafricatv) 's Twitter Profile Photo

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Kagera Kamishna Msaidizi Zabron Muhumha amesema watu wanne wa wilayani Ngara mkoani Kagera wamefariki kwa ajali ya moto na wengine 7 wamenusurika baada ya nyumba waliyolala kuungua moto usiku wa kuamkia leo.

kila Jumatatu…

account_circle
EastAfricaTV(@eastafricatv) 's Twitter Profile Photo

Athari za mvua zimeendelea kuonekana Afrika Mashariki ambako sasa Kenya imeripoti kuongezeka kwa idadi ya watu waliopoteza maiasha kutokana na mafuriko imefikia 43 baada ya miili 3 zaidi kupatikana kwenye mto Mathare, Kaunti ya Nairobi.

kila Jumatatu - Ijumaa
Saa…

account_circle
EastAfricaTV(@eastafricatv) 's Twitter Profile Photo

WAHITIMU WA ELIMU YA DINI WATAKIWA KUPAMBANA NA MMOMONYOKO WA MAADILI

Wahitimu wa dini nchini wametakiwa kuwa vinara katika mapambano dhidi ya mmomonyoko wa maadili ili kuweza kuwa na jamii bora yenyenustawi.

account_circle
EastAfricaTV(@eastafricatv) 's Twitter Profile Photo

Kijana anayefahamika kwa jina la Shaban Athuman Mgosi (39) mkazi wa Majengo Mapya mjini Moshi ameuawa leo saa 12:20 asubuhi baada ya ugomvi baina yake na rafiki yake kwa kile kinachodaiwa kutaka kudhulumu simu.

cc Gerald Michael Nyang'ali

account_circle
EastAfricaTV(@eastafricatv) 's Twitter Profile Photo

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Tundu Lissu, amewaomba watanzania kujitokeza katika maandamano yanayoandiliwa na chama hicho ili kuunganisha nguvu kwa pamoja kwa ajili kudai Katiba Mpya. Tundu Antiphas Lissu

kila Jumatatu - Ijumaa
Saa 1:00-2:00 Usiku

account_circle
EastAfricaTV(@eastafricatv) 's Twitter Profile Photo

MLIMA HANANG WALETA MAFURIKO TENA

Taharuki imezuka tena kwa wananchi wa kijiji cha Gocho kata ya Giting-Hanang baada ya sehemu ya Mlima Hanang kwa mara nyingine tena imeporomoka na kusababisha mafuriko ya maji na kuharibu mazao na makazi ya watu wa kijiji cha Gocho

account_circle
EastAfricaTV(@eastafricatv) 's Twitter Profile Photo

WANANCHI WAOMBA WANAOJIUZA WACHUKULIWE HATUA

Wananchi wilayani Ilemela mkoani Mwanza wametaka hatua za maksudi kuchukuliwa ili kukomesha shughuli za kujiuza nje ya uwanja wa CCM Kirumba wakidai eneo hilo limegeuka danguro nyakati za usiku.

account_circle
EastAfricaTV(@eastafricatv) 's Twitter Profile Photo

WALIOFARIKI KWA MAFURIKO MOSHI WAAGWA
Miili ya watu waliofariki kwa mafuriko wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro imeagwa leo katika viwanja vya Halmashauri ya Wilaya hiyo na Mamia ya waombolezaji.

account_circle
EastAfricaTV(@eastafricatv) 's Twitter Profile Photo

NILITAMANI SANA MDOGO WANGU (NOEL) APONE - FESTO RICHARD SANGA

Vijana wametakiwa kuachana na mambo ya dunia na kumrudia Mungu kwani changamoto za maisha zimekuwa nyingi hivyo kwa kumrudia Mungu kutawasadia kukabiliana nazo.

kila Jumatatu - Ijumaa
Saa 1:00-2:00 Usiku

account_circle